Mbunge wa jimbo la Mafinga
Mjini Cosato Chumi kulia akisikiliza kilio cha wafanyakazi wa zahanati na vituo vya afya alipotembelea kujionea na kusikiliza changamoto za huduma za afya katika jimbo lake ili kuzitafutia ufumbuvi na kuboresha huduma hiyo.


Na fredy mgunda,Iringa
MBUNGE wa jimbo la Mafinga Mjini
Cosato Chumi alifanya ziara ya kuzitembelea zahati,vituo vya afya na hospitali
za jimbo hilo kwa lengo la kujionea changamoto za kiafya. 

Akiwa katika ziara hiyo
alikumbana na changamoto ya kukosekana kwa umeme katika baadhi zahati za jimbo
hilo na kuahidi kulipeleka tatizo hilo bungeni ili litafutiwe ufumbuzi mapema.

Akizungumza na blog hii
Chumi alisema tatizo la umeme katika vituo na zahati ni kubwa hivyo inahitajika
nguvu ya ziada kutatua tatizo la umeme ili kuboresha afya za wananchi wake
pamoja na huduma ya mama na mtoto.

“Hii inasikitisha sana hebu
angalia zahati zinavifaa vyote mhimu ila umeme ndio tatizo hatuwezi kupata
huduma bora kama hakutakuwa na umeme tunaelekea bungeni nitaenda kuongea na
waziri husika ili kutatua changamoto hii” alisema Chumi

Aidha mh chumi alisema kuwa
anapenda kuhakikisha kuwa umeme wa REA awamu ya tatu unazifikia zahati zote
pamoja na vijiji husika kwa kuwa serikali inalengo la kusambaza umeme vijiji
vyote nchi nzima hivyo hata vijiji vya jimbo la Mafinga Mjini vimo katika
mpango huo.

Nao baadhi ya Wananchi
walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya kuwaletea maendeleo katika
jimbo la Mafinga Mjini ndani ya mwaka mmoja tu amefanya vitu vingi vizuri
tofauti na matarajio ya watu wengi.

“Angalie nyie waandishi wa
habari Mbunge Cosato Chumi kwa mwaka moja tu ametengeneza barabara karibi a
zote za jimbo huku nyingine zikiwekwa rami,amehangaikia swala la maji tunaona
matumaini,swala afya ndio kafanya vitu vingi,michezo ndio mechi zinaendelea na
mambo mengine mengi huyu mbunge ni wakuigwa kwa juhudi zake” walisema wananchi

Wananchi hao waliongeza kuwa
swala la umeme mbunge wetu ametueleza vizuri sana hivyo tunaimani ya maneno na
vitendo yake kuwa analishughurikia kwa umuhimu mkubwa.

Baadhi ya madiwani wa jimbo
hilo walisema kuwa kuwa mbunge huyo amekuwa akiwasaidia kutatua changamoto
nyingi za kitendaji na kuifanya kazi yetu ya udiwani kuwa rahisi kutokana na
mambomengi anayafanya mbunge wetu Cosatio chumi.

“Tunamshukuru Mbunge wetu
kwa kuwasaidia wananchi taa za sola kwa vijiji ambavyo havina umeme hizo ni
juhudi zake binafsi na sio hilo kafanya mambo mengi sana hadi sasa tunajiona
tupo kwenye halmashauri kongwe kumbe ni halmashauri mpya” walisema baadhi ya
wadiwani 

Kwa upande wake mwenyekiti
wa halmashauri ya Mji wa Mafinga Charle Makoga amesema kuwa changamoto ya umeme
ni kubwa katika vijiji ambavyo havipokupata umeme wa REA awamu ya kwanza na
pili na ndio sababu inayosababisha huduma za kiafya kudorola katika baadhi ya
vijiji
.