Klabu ya Tottenham Hotspurs iliandikisha ushindi mkubwa na kuwawekea presha viongozi wa ligi ya Uingereza Chelsea baada ya kuicharaza Watford mabao 4-0.
Mabao hayo yalifungwa na Dele Ali, Son Heung aliyefunga mawili na Eric Dyer.

Ushindi huo ni wa sita kwa upande wa vijana hao wa kocha Pochetino.
Watford walianza vizuri kwa kutishia lango la Hotspurs kabla ya mambo kubadilika.
Nayo klabu ya Manchester City ilisitisha matokeo mabaya ya mechi nne mfululizo kwa kuilaza Hull City 3-1 hatua inayopiga jeki harakati za kufuzu katika kombe la vilabu bingwa Ulaya.
Mabao ya Manchester City yalifungwa na Sergio Aguero, Delph huku kipa wa Hull City Ahmed Elmohamady akijifunga.
Wakati huohuo timu ya Liverpool ilitoka nyuma na kuilaza Stoke City kupitia mabao yaliofungwa na Phillipe Coutinho na Roberto Firmino.
Stoke City ilikuwa imeongoza baada ya Jon Walters kufunga krosi iliopigwa na Xherdan Shaqiri.