Kura za awali nchini Ujerumani katika jimbo lenye idadi kubwa ya watu liitwalo North Rhine-Westphalia zimeonyesha kuwa chama cha bi Angela Merkel cha Christian Democrats kinaongoza kwa kishindo.

Wanatabiriwa kushinda zaidi ya asilimia 34 ya kura zote wakiwazidi wapinzani wao wa karibu ambao ni chama cha Social Democratic party.
Matokeo hayo yanaonekana kama pigo kwa chama cha upinzani cha Social Democratic kwa uchaguzi mkuu wa mwezi Septemba ambapo pia katika jimbo hilo wanapachukulia kama nyumbani.
Kiongozi wa chama hicho Martin Schulz amesema ni uchungu sana kushindwa katika jimbo la nyumbani.
Schulz alichukua uongozi wa chama hicho mapema mwaka huu.