Hull City waliondolewa kutoka Ligi ya Premier wakiwa na mecchi moja ya kucheza kufuatia kipigo kikali walichopewa na Crystal Palace.
Kikosi hicho cha Marco Silva kilipigwa na mshutuko na bao la dakika mbili na sekunde 11 baada ya kuanza kwa mechi.
Mlinzi raia wa Italia Andrea Ranocchia alishindwa kuondoa mpira eneo la hatari hali iliyompta fusra Wilfried Zaha kutikiza wafu wa Hull City.
Bao la pili la Christian Benteke lilitimiza mabao mawili ya Crstal Palace huku mabao mengine mawili yakifungwa na Luka Milivojevic, na Patrick van Aanholt.
Sasa Hull watajiunga na Sunderland pamoja na Middlesbrough kusubiri msimu unaokuja.
|
0 Comments