Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard Kasesela akiwa na viongozi
mbalimbali wa Manispaa ya Iringa kama Naibu Meya Joseph Lyata na
mbunge wa viti Maalum mkoa wa Iringa kupitia chama cha mapinduzi CCM
Ritta Kabati wakisikiza hoja za wananchi wa Kata ya mlandege



Na Fredy Mgunda,
Iringa




Watendaji wa kata ya mlandege
wamepewe wiki mbili kuitisha mikutano ya kusoma mapato na matumizi ya
kila mitaa ili kupunguza na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi
wao.


Akizungumza
wakati wa mkutano wa hadhara Mkuu wa Wilaya ya Iringa Richard
Kasesela aliwataka viongozi kufanya kazi kwa umakini na kuitisha
mikutano ya hadhara kwa wakati ili kupunguza kero
zinazowakabili.


"Wananchi wa Kata hii wanakero
nyingi ambazo viongozi wa Kata mnaweza kuzitatua sio lazima zinifikie
mimi huku,nawaombeni sana viongozi fanyeni kazi la sivyo
nitawachukulia hatua mara moja"alisema Kasesela


Kasesela alisema kuwa kata ya
mlandege haina changamoto nyingi ili changamoto hizo zinasababishwa na
viongozi wa Kata kwa kutofanya mikutano ya hadhara kwa
wakati.


Aidha Kasesela alisema kuwa
ataendelea kutatua kero zote kwa wananchi kwa kuwa yeye ni kiongozi wa
wananchi na ameletwa na Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dr
John Pombe Magufuli kufanya kazi kwa wananchi.


Kero nyingine zilizokuwa hapa
Kata ya mlandege zitatatuliwa wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa
atazitatuwa kulingana na mipango iliyopo
 serikalini.

Kasesela alimuomba mbunge wa
viti maalumu mkoa wa Iringa Ritta Kabati kuzipeleka bungeni baadhi
kero ambazo zipo juu ya uwezo wao kama kero ya maji,ardhi na swala
Mipangomiji.


Kwa upande wake mbunge wa viti
Maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati alisema kuwa ameyapokea na
anayapeleka bungeni kuyatatua matatizo na kuyatafutia ufumbuzi wa kero
za wananchi.


"Nimekuja hapa kwenye mkutano
hadhara kuzichukua kero hizi ili nizipeleke sehemu husika na mimi
nitafanya kazi kwa kujituma ili kuisaidia Manispaa ya Iringa kuwa na
maendeleo ya haraka sana"alisema Kabati


Naye Mkurugenzi wa Manispaa ya
Iringa dr mafwele alisema kuwa amezisikia kero zote na atazifanyia
kazi kwa umakini mkubwa ili kuboresha maisha ya wananchi wa Manispaa
ya Iringa.
.