Michuano ya kombe la dunia la vijana chini ya umri wa miaka 20 inaendelea kushika kasi huko nchini Korea ya kusini ikiwa katika ngazi ya makundi.
Katika michezo ya kundi C wawakilishi wa Afrika timu ya Zambia walipata ushindi mabao 4-2 dhidi ya timu ya Iran. Nao Costa Rica wakatoshana nguvu na Ureno kwa Sare ya bao 1-1.

Kwenye kundi D Afrika ya kusini walichapwa na Italia kwa mabao 2-0, huku Uruguay wakiwafunga Japani kwa 2-0.
UruguayHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKikosi cha timu ya taifa ya Uruguay
Michuano hiyo inaendelea tena leo katika kundi E Ufaransa watacheza na Vietnam, na New Zealand wakipepetana na Honduras.
Katika kundi F Ecuador wataonyesha ubavu na Saudi Arabia, huku Senegal wakicheza na Marekani.