Al ustadh Habib akitoa mawaidha kuhusu mfungo wa Ramadhani na akisisitiza mambo ya upendo katika jamii ya mwanadamu na maisha yake ya kila siku.

Muda wa Iftari ulipowadia kila mmoja wetu alipata rizik

Waumini wakiendelea kupata riziki "Alla Akbar"

Na kwa upande wa kina mama "mash'Allah" kila idara ilijipanga vyema katika kuhakikisha watu wote wanapata chakula ipasavyo

Big brother Salmin akihakiki chupa zote za vinywaji moto vipo sawasawa "Allah Karim"

Azan ilipoadhiniwa kila mmoja alifungulia swaumu yake na kitu alichopenda,pichani mama Denzel akifungua kinywa na juisi"Mash'Allah"

Mabinti wa Mol ambao ndio mama zetu wa kesho nao wakiwa pamoja wakisubiri muda wa Iftar "Mash'Allah"

Wageni na waumini wakifungua kinywa "Alhamdulillah"

Mzee wetu Al-Haj Mzee Bales akipata matunda kama kifungua kichwa chake "Allah Karim"

Mama Karim akipata Iftar" Mash' Allah"

Ustadhi Nyambi akiendelea kutoa huduma kwa waumini

Brother Omar akipata rizik

Waumini na watoto wakipata rizik

Mash'Allah malaika wa Mungu nao waliojaaliwa kufunga wakipata rizik

Uislam na taratibu zake ukichukua nafasi,hapo Waumini wakisubiriana kwenye mstari wa chakula

Masha'Alla vijana wakipata Iftar

Mume wa Rahma ama Ally van Rahma mwenye kanzu ya bluu akipata Iftar

"Allah Karim" waumini wakiendeleza sunna ya Iftar

Mash'Allah Mash'Allah 

Kiungo muhimu Al habib Jamal akifurahia Iftar "Allah Akbar"

Mash'Allah 
Mash'Allah dada yetu kipenzi toka Hasselt pia nae alikuwepo
Shekh Yusuf akiweka kipaza sauti sawasawa ili shekh Abdallah aweze kuchangia mawili matatu kwenye mawaidha ya Ramadhani hapo jana

Baada ya Iftar kina mama wakipata mawaidha"Mash'Allah".{Picha zote na Maganga One Blog}


Assalam Aleykum,Baada yakumshukuru Mwenyezi Mungu na kumtakia rehema na Amani Mtume wetu kipenzi Muhammad Sallah lallahu Aleyh Wassallam,Wana Mol na Uongozi mzima hatuna budi kumshukuru kila mmoja wetu aliyekubali mualiko wa Iftar hapo jana.Tunatoa shukrani zetu za dhati kabisa kwa wale wote waliofika kujumuika nasi na pia tunatoa shukrani zetu pia kwa wale wote walioshindwa kuja kwa namna moja au nyingine na  in sha Allah wakijaaliwa siku zijazo tutajumuika nao.

Wana Mol wanasisitiza upendo kwa Waislam wote duniani na kuwatakia mfungo mwema kwa siku zilizobaki za Ramadhani.
Wabillah Taufiq
Uongozi.