Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewasili usiku huu Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo hapo kesho tarehe 03 Julai 2017 atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa  Nchi na Serikali  wa Umoja wa Afrika (AU).Mhe.Samia 
amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ethiopia Pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Naimi Aziz na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga mara baada yakuwasili jijini Addis Ababa,nchini Ethiopia usiku huu. 

Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassa akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne wa Tanzania,Dkt JakayaKikwete mara baada yakuwasili jijini Addis Ababa mapema usiku huu

Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
amewasili usiku huu Jijini Addis Ababa, Ethiopia ambapo hapo kesho
tarehe 03 Julai 2017 atahudhuria Mkutano wa 29 wa Wakuu wa  Nchi na
Serikali  wa Umoja wa Afrika (AU).

Katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Bole Jijini Addis Ababa Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu
Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Ethiopia Pamoja
na Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Naimi Aziz na Waziri wa Mambo ya
nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt Augustine Mahiga.

Katika
Mkutano huo wa siku mbili kuanzia tarehe 03-hadi 04 Julai-2017, Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan
atamuakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwenye mkutano huo.

 Kabla ya ufunguzi rasmi, Mkutano
huo ulitanguliwa na vikao vya Baraza la Utendaji linalowashirikisha
Mawaziri wa Mambo ya Nje na Kamati ya Uwakilishi wa Kudumu 
inayowahusisha Makatibu Wakuu wa Wizara za Mambo ya Nje kutoka nchi
Wanachama wa Umoja wa Afrika.

Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi  na
Serikali  utafunguliwa rasmi kesho tarehe 03-Julai-2017 katika Makao
Makuu ya Umoja wa Afrika Jijini Addis Ababa, Ethiopia na  utajikita
katika kujadili masuala mbalimbali yanayohusu umoja huo.

Miongoni
mwa mambo yatakayojadiliwa katika Mkutano huo ni pamoja na taarifa 
kuhusu Maboresho katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na
maboresho ya kitaasisi katika AU na  hali ya Ulinzi na Usalama katika
bara la Afrika.

Kuhusu  hali ya  ulinzi na usalama katika Bara la
Afrika majadiliano ya Viongozi hao yatajikita zaidi kwenye nchi za
Sudan Kusini, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo- DRC na Libya. 
Aidha, majadiliano hayo pia yatagusa  hali ya usalama kwenye baadhi ya
nchi ambazo ziliathiriwa na kundi la Boko Haram za  Nigeria, Niger, Chad
na Cameroon.

Mkutano huo 29 wa AU, unatarajiwa kuhuduhuriwa na
viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio
Guterres na Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas.

Mkutano
huo 29 wa AU utakaofanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia utaongozwa na
Mheshimiwa  Alpha Conde  Rais wa Jamhuri ya Guinea ambaye ndiye
Mwenyekiti wa AU.

Kauli Mbiu ya Mkutano huo ni Kuimarisha
Mgawanyiko wa Idadi ya Watu Kupitia Uwekezaji katika Vijana (Harnessing
Demographic Divident Through Investments in the Youth)

Imetolewa na

Ofisi ya Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 ADDIS ABABA- ETHIOPIA.      

03-Julai-2017