Follow us: Subscribe via RSS Feed Connect on YouTube Connect on YouTube
Maganga One Blog kwa habari za kitaifa,kimataifa,burudani na michezo kila siku. Tutumie habari na matukio yoyote kwa email yetu ya magangaone@gmail.com

Aug 2, 2017

Ngoma Africa Band walivyoliamsha Dude mjini Bonn,Ujeruman

JINAMIZI LA MZIKI WA DANSI BADO LINATESA ULAYA
Ngoma Africa band aka Viumbe wa ajabu aka FFU-Ughaibuni ni tishio !
Mara nyingi wamekuwa na tabia za kuteka maelfu ya washabiki kwa kutumia mdundo wao "extraordinary Bongo Dansi" ambao umeifanya bendi hiyo maarufu barani ulaya kujiwekea nafasi ya pekee katika majukwaa ya kimataifa, siku ya ijumaa ya tarehe 28-7-2017 katika ya jiji la Bonn ,nchini Ujerumani bendi hiyo ilifanikiwa kwa mara nyingine kuhakikishia ulimwengu
kuwa muziki wake ni moto wa kuotea mbali,pale ilipofanikiwa kuwatia kiwewe washabiki wake hadi washabiki kuwazidi nguvu walinzi nakucheza hadi jukwaani,bendi hiyo inayoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja imejijengea himaya ya washabiki wake kila kona,Ngoma Africa band ina wanamuziki wenye vipaji na walioipindia akili kazi yao ya kudatisha washabiki,kikosi kazi hiko kimebandikwa majina mengi ya kisanii yakiwemo Viumbe wa ajabu majinamizi"Anunnaki Aliens" , au "Watoto wa Mbwa" pia maarufu kama FFU-Ughaibuni majina hayo yanatokana na tabia zao wawapo jukwaani.
Share this article :

0 Maoni:

 
Maganga One Blog © Copyright 2017. All Rights Reserved.

Powered by Maganga One.
Back to TOP