Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza jambo wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akikagua mtambo wa uchongaji mashimo kwa ajili ya utafiti wakati alipotembelea Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.

Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akisitiza wakati wa kikao cha pamoja na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko akiwa katika picha ya  pamoja na Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Mtaa wa Upanga Jijini Dar es salaam, Leo 16 Januari 2018.

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Uongozi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) umetakiwa kutoa
maelezo kwa serikali katika kipindi cha muda mfupi kueleza sababu za kuendelea
kusalia kuwepo kwa shirika hilo kutokana na kukosa umakini katika utendaji.

Kauli ya kuchukizwa na utendaji wa Shirika hilo imetolewa Leo 16
Januari 2018 na Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Dotto Mashaka Biteko
Wakati akizungumza na Uongozi pamoja na watumishi wa Shirika hilo Mtaa wa
Upanga Jijini Dar es salaam.

Mhe Biteko alisema kuwa serikali ilikuwa na makusudi mazuri
kufuatia mabadiliko ya Sera za kiuchumi katika miaka ya 1980 kwa STAMICO
kuwekwa kwenye orodha ya mashirika yanayotakiwa kubinafsishwa na hatimaye
kubinafsishwa rasmi mwaka 1996 lakini katika kipindi chote cha utendaji hakuna
msaada wowote ambao Shirika hilo limeipatia serikali zaidi ya kuingiza hasara
maradufu.

Alisema kuwa pamoja na STAMICO kuwa na jukumu la kuendeleza
migodi ya Madini na kufanya biashara za Madini ikiwemo mradi wa dhahabu wa
STAMIGOLD uliopo Biharamlo Mkoani Kagera na Mgodi wa Makaa ya Mawe KABULO
uliopo Mkoani Ruvuma lakini Taasisi hiyo imeshindwa kuendeleza migodi kwa
ufanisi huku wachimbaji wadogo wakisalia kuwa katika uduni wa mbinu rafiki na
tija katika utendaji kazi wao.

Alisema kuwa Shirika hilo linapaswa kutafakari kwa umakini
utendaji wake kwani limeongeza hasara kwa serikali ya deni la shilingi Bilioni
1.77 hivyo serikali haiwezi kuendelea kusalia kuwa na Shirika linalozalisha
madeni kuliko matokeo makubwa na faida.

Aliongeza kuwa wataalamu wote katika sekta ya Madini wanapaswa
kutambua kuwa biashara ya Madini ni zaidi ya kutoa leseni hivyo watambue kuwa
kuna kila sababu ya kuwa na matumizi bora ya mapato na kutazama namna bora ya
kuifanya sekta ya Madini kuchangia asilimia 10% ya pato la Taifa.

Mhe Biteko alisema kuwa imani bila matendo ni uduni wa fikra
hivyo kuwa na cheo kikubwa serikalini halafu uzalishaji ni mdogo ni kipimo
halisi cha utendaji wa mazoea walionao watumishi wengi ambao wamekosa uzalendo
na bidii katika utendaji kazi.

Alisema kuwa serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imekusudia
kusimamia vyema rasilimali za wananchi hivyo watendaji katika sekta mbalimbali
wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kumsaidia Rais Magufuli katika kuteleleza
adhma ya serikali.

MWISHO