Rais wa Afrika Kusini , Cyril Ramaphosa, amekatisha ziara yake alipokuwa kwenye mkutano wa jumuiya ya madola nchini Uingereza ili kukabiliana na maandamano na vurugu nchini mwake.
Rais Ramaphosa aliitumia ziara yake kujaribu kuwashawishi baadhi ya wajumbe wa mkutano huo kuwekeza nchini mwake, ziara hii ni ya kwanza kimataifa baada ya kutwaa madaraka kutoka kwa raisi mstaafu Jacob Zuma mnamo mwezi Februari mwaka huu.
Lakini mapigano yameongezeka zaidi ya siku mbili katika jimbo la Kaskazini Magharibi.waandamanaji wanadai fursa ya ajira na makaazi na pia wanataka kuona rushwa inakomeshwa nchini mwao.
Barabara zimefungwa, magari yanachomwa moto na maduka yanavunjwa hovyo na wakaazi wa eneo hilo wametoa wito wa kujiuzulu kwa waziri mkuu wa jimbo.
Rais Ramaphosa amewataka waandamanaji kutulia na kuwataka polisi kuanza zoezi la kuzuia maandamano mapya.
|
0 Comments