Baadhi ya watuhumiwa wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo wakiwa wameficha sura zao wamefika mahakamani hapo kwaajili ya kujibu tuhuma mbalimbali ikiwemo tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.
 
Gari la Jeshi la Polisi likiwafikisha watuhumiwa wa makosa mbalimbali ikiwemo ya watumiaji wa maudhui ya matandao bila kibali. 


Baadhi ya watuhumiwa wakiwa wameficha nyuso zao baada ya kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo, kwa  kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Na Karama Kenyunko, blogu ya jamii

MTANGAZAJI wa Clouds na mmiliki wa mtandao wa Shafii Dauda,  Shafii Dauda Kajuna na Benedict Kadege  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kutumia maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali.

Wakili wa Serikali Mkuu Tumaini Kweka akisaidiana na mawakili Mutalemwa Kishenyi na Mwanaamina Kombakono wamewasomea washtakiwa shitaka lao mbele ya Hakimu mkazi Mfawidhi Kelvin Mhina
Akiwasomea hati ya mashtaka Wakili Kombakono amedai kuwa  kati ya Juni 14 hadi Septemba mwaka huu ndani ya Jiji la Dar es Salaam kwa kutumia online Tv inayojulikana kwa jina la Shafii Dauda, washtakiwa kinyume cha sheria walitoa maudhui katika mtandao huo bila ya kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Hata hivyo, baada ya kusomewa shtaka hilo washtakiwa hao wamekana huku upande wa mashtaka ukidai upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.
Hata hivyo Wakili Jebra Kambole anayewatetea washtakiwa hao aliomba Wateja wake hao wapewe dhamana kwa sababu shtaka wanaloshtakiwa nalo linadhaminika.

Wakili Kweka amedai kuwa hawaping kutoa dhamana bali kama mahakama itaridhia kutoa dhamana izingatie kifungu cha 148 (6)(7) cha sheria ya makosa ya jinai.

Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Mhina alimtaka kila mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili kwenye kitambulisho vya kuwatambulisha na barua ambazo zinatambulika.

Pia kila mdhamini alitakiwa kusaini bondi ya Sh .milioni 15 na hawaruhusiwi kusafirisha nje ya Tanzania bila kupata kibali cha mahakama.

Pia wametakiwa kuwasilisha hati zao za kusafirisha mahakamani Oktoba 8 mwaka huu.