Mabingwa watetezi Cameroon na wenyeji Misri wameyaaga mashindano Jumamosi Juni 6 baada ya kutolewa kwenye siku ya pili ya hatua ya mtoano.
Cameroon na Misri ndio waliocheza fainali ya Kombe la Maifa ya Afrika (Afcon) miaka miwili iliyopita ambapo Cameroon ilitwaa ubingwa.

Hata hivyo timu hizo mbili zimeyaaga mashindano baada ya Cameroon kufungwa 3-2 dhidi ya Nigeria jijini Alexandria.
Misri wamepigwa mbele ya mashabiki elfu sabini jijini Cairo na Afrika Kusini kwa goli moja tu lililofungwa na Thembinkosi Lorch katika dakika ya 85.
Afrika Kusini ambao walifuzu katika raundi ya mtoano kama timu ya tatu kwenye kundi lao baada ya kushinda mchezo mmoja tu haikupigiwa upatu katika mechi ya leo dhidi ya Misri inayoongozwa na mshambuliaji wa Liverpool Mo Salah.
Umakini wa safu ya ulinzi wa Afrika Kusini hii leo ndio imekuwa chachu ya ushindi baada ya kuhimili vishindo na mikiki ya safu ya ushambuliaji ya Misri ambayo iliibuka na ushindi kwenye mechi zote tatu za makundi.
Mchezaji wa Nigeria, Wilfred Ndidi alisema kabla ya mchezo kuwa huenda Cameroon akawa mpinzani mwepesi kuliko Madagascar, iliyowashinda katika mechi ya mwisho katika makundi.
Naam, Nigeria ilianza kwa kasi mchezo huo na kutangulia kupata goli katika dakika ya 19 kupitia Odion Ighalo.
Cameroon wakajibu mapigo kama Simba aliyejeruhiwa na kupata magoli mawili ya haraka kupitia Stephane Bahoken na Clinton N'Jie.
Katika kipindi cha pili, Nigeria ikarudi kumaliza mchezo.
Ighalo alipachika goli la kusawazisha katika dakika ya 63 na dakika tatu baadae, Ighalo akamtengea Alex Iwobi pasi safi aliyoiunganisha na kupachika bao la ushindi kwa Nigeria
Nigeria vs Afrika Kusini
Timu ya taifa ya Nigeria imerudi katika mashindano hayo baada ya kukosekana katika awamu mbili zilizopita za mashindano hayo, mnamo 2017 na 2015.
Wamerudi mara hii chini ya ukufunzi wa kocha Gernot Rohr.
Odion Ighalo ndiye mfungaji mkuu katika mechi za kufuzu mashindano ya mwaka huu, akiifungia timu hiyo mabao 7. Ighalo baada ya mechi ya leo anafikisha goli tatu kwenye mashindano haya.
Afrika Kusini wao walionekana wakiingia uwanjani hii leo kwenda kupoteza mbele ya wenyeji Misri ambao wengi walidhani wangeweza kulibakisha kombe nyumbani.
Hata hivyo, kocha wa Afrika Kusini Stuart Baxter kabla ya mchezo alisema kuwa amewaandaa wachezaji wake dhidi ya shinikizo la kucheza mbele ya mashabiki wa Misri watakaojaa uwanjani.
Pasi na shaka katika hilo mbinu za Baxter zimefuzu.
Sasa Nigeria na Afrika Kusini zitaminyana katika mchezo wa robo fainali wiki ijayo.
Nani kuibuka na ushindi na kusonga nusu fainali? Muda utaongea.
MASHABIKI WA CAMEROONHaki miliki ya pichaCAF
Mashabiki wa Super Eagles NigeriaHaki miliki ya pichaJONATHAN TORGOVNIK
Image captionMashabiki wa Super Eagles Nigeria
Nigeria 3
-
2 Kameruni
Muda kamili
Mbinu
Nigeria
4-2-3-1
Kameruni
4-2-3-1
Taarifa
  • 19
    -
    Ighalo
     
    1 - 0
  • 28
    -
    Kunde
     
    1 - 0
  • 41
    -
    Bahoken
     
    1 - 1
  • 44
    -
    N'Jie
     
    1 - 2
  • 51
    -
    Mandjeck
     
    1 - 2
  • 60
    -
    Chukwueze
     
    Simon
     
    1 - 2
  • 62
    -
    Zambo Anguissa
     
    Mandjeck
     
    1 - 2
  • 63
    -
    Ighalo
     
    2 - 2
  • 66
    -
    Iwobi
     
    3 - 2
  • 70
    -
    Awaziem
     
    3 - 2
  • 70
    -
    Toko Ekambi
     
    N'Jie
     
    3 - 2
  • 85
    -
    Paul Onuachu
     
    Ighalo
     
    3 - 2
  • 87
    -
    Zoua
     
    Kunde
     
    3 - 2
  • 91
    -
    Balogun
     
    Iwobi
     
    3 - 2