Mchezaji nyota wa Liverpool Sadio Mane ameisaidia Senegal kutinga robo fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kuilaza Uganda bao 1-0.
Bao hilo la ufunguzi lilitiwa wavuni na Mane katika dakika za mwanzo wa kipindi cha kwanza liliashiria mwanzo mzuri kwa Senegal katika kampeini yake kuelekea fainali ya kipute hicho.
Timu hiyo imeonesha mchezo mzuri tangu mwanzo wa mashindano haya japo ilinyukwa na bao 1-0 na Algeria katika mechi ya makundi.
Mchezaji Idrissa Gueye - anayesakata soka ya kulipwa katika klabu ya Everton alionesha uhodari wake katika mechi hiyo kwa kudhibiti safi ya kati peke yake na kuongoza kasi ya mchezo kwa wachezaji wenzake.
Uganda ilifanya makosa mengi na kukosa uwezo wa kiufundi wa kudhibiti mchezo huo. Uganda pia ilifanya makosa mengi ya ulinzi katika mashindani ya kiwango hiki iliyosababisha wafungwe bao huku Mane akipoteza penati dhidi yao.
Uganda imeondolewa katika mashindano hayo lakini wachezaji wake waliiweka taifa hilo mbele kwa kuonesha mchezo mzuri na pea talata ya wachezaji wake.
Senegal imeondoa timu zote za Afrika Mashariki ambapo ilianza na Tanzania, Kenya na sasa Uganda.
Kwa upande wake Benin iliichapa Morocco mabao 4-1 kupitia mikwaju ya penati na kujikatia tiketi ya robo fainali ya michuano hiyo.
Mama Seibou ndiye aliyeweka kimyani penati ya ushindi na kuisogeza mbele timu ya Benin iliyokuwa na wachezaji 10 baada ya Khaled Adenon kutolewa uwanjani katika muda wa ziada wa mchezo huo.
Katika mechi hiyo ya kusisimua uliyochezwa mjini Cairo, Moise Adilehou aliiweka Benin kifua mbele kabla ya Youssef En-Nesyri kusawazisha bao hilo.
Morocco walikua na nafasi ya kushinda katika muda wa kawaida lakini penati ya Hakim Ziyech iligonga mlango wa goli na mpira ukatoka nje.
Benin walifunga penati zao zote kupitia wachezaji Olivier Verdon, David Djigla na Tidjani Anaane kabla ya juhudi za Seibou kukamilisha mechi hiyo kwa shangwe kubwa nje na ndani ya uwanja wa Al Salam.
Benin ambao wanashiriki kwa mara ya nne mashindano ya Afcon sasa watakipiga na Senegal katika awamu ya ribo fainali itakayochezwa Julai 10.
|
0 Comments