Katika utafiti wa zaidi ya watu 3,400 nchini Marekani wanaosoma shahada ya kwanza, wale waliosema wana matatizo na muda wanaotumia katika simu zao wanaripotiwa kuwa na wapenzi wengi pia.
Na wanadhaniwa kuwa na msongo wa mawazo, mmoja wa watafiti amesema kuwa matokeo yautafiti yanashangaza.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha Chicago, Cambridge na chuo kikuu cha Minnesota wamefanya tafiti hii ya tabia za uraibu wa simu.
Lengo la utafiti huu lilikua ni kutaka kujua hali ya afya ya akili ya wanafunzi na jinsi gani simu zina matokeo katika utendaji wao.
Ili kujua matumizi yaliyopitiliza ya simu za mkononi, wanafunzi waliulizwa maswali mbalimbali ikiwemo yafuatayo;
Rafiki zako na familia wanalalamika hukusu matumizi makubwa ya simu?
Una matatizo yoyote darasani kutokana na matumizi ya simu?
Unadhani muda unaotumia simy umeongezeka?
Mwanafunzi mmoja kati ya watano miongoni mwa waliojibu maswali walikubali maswali yote, na kuwafanya kuwa watumiaji wa kupitiliza wa simu, miongoni mwao wengi ni wanawake.
Kuacha mahusiano ya kawaida
Kwa hao wenye matumizi yaliyozidi ya simu za mkononi, wameripotiwa pia na uhusiano wa kimapenzi na zaidi ya mwenza mmoja katika kipindi cha miezi 12, kuliko wale waliokutwa hawana matumizi makubwa ya simu.
Alisilimia 37.7 ya wenye uraibu wa matumizi ya simu, wamekadiriwa kuwa na wapenzi hadi sita ndani ya miezi 12. Ikilinganishwa na asilimia 27.2 ya walioripotiwa kutokua na tatizo ya matumizi makubwa ya simu.
Dkt. Sam Chamberlain, mmoja kati ya waandishi wa tafiti hii kutoka chuo kikuu cha Cambridge anasema sababu ya suala hili ni ngumu kuijua.
''Inawezekana kuwa watu wanatumia sana simu na kukutana na wapenzi mtandaoni na wanaweza pia kusahau mahusiano ya kila siku kwa sababu ya matumizi yaliyokithiri ya simu za mkononi.''
"Kama hili suala lingekua na faida basi ingekua kinyume na matokeo badala yake afya ya akili ingekua imeimarika," ameongeza Dkt. Chamberlain.
Watafiti pia waligundua unywaji wa pombe kupita kiasi unawakumba wale wanaotumia simu kwa muda mrefu zaidi. Lakini hawakukutwa na uraibu mwingine wowote.
Baadhi ya wataalamu wamependekeza kuwa uchezaji wa 'game', ambao umewekwa katika kundi la tatizo na Shirika la Afya Duniani, ijumuishwe pia tatizo la kukaa muda mrefu katika vioo vya simu.
Tafiti za nyuma zimeonesha uhusiano wa kufeli kwa wanafunzi na matumizi ya simu, na ripoti hii pia ina uhusiano na suala hilo.
"Hata kama kuwa matokeo ya tatizo hili, yana madhara yake katika taaluma ya mtu na baadae katika kipindi chake cha kufanya kazi," amesema Profesa Jon Grant wa chuo kikuu cha Chicago.
Dkt Abigael San amesema kuwa anafurahia utafiti huu umefanyika: "haya madhara yote ni ya kweli na tunatakiwa kuyazingatia, watu wengi wanaweka tatizo hili kama tatizo la afya ya akili ama kuvunjika kwa mahusiano, lakini hayo yote yanachangiwa na matumizi ya simu za mkononi."
0 Comments