Klabu ya AS Vita ya DR Congo imealikwa kucheza na Yanga siku ya utambulisho wa kikosi cha timu hiyo ambayo ni siku ya kilele cha wiki ya Mwananchi.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela amesema mchezo huo utapigwa Agosti 4, 2019 katika Uwanja wa Taifa.


Awali Yanga ilipanga kufanya tukio hilo Julai 27, hata hivyo kutokana na muingiliano wa ratiba na timu ya Taifa, sasa litafanyika Agosti 4, 2019.