Rais wa Uganda Yoweri Museveni anatarajiwa kuzuru nchini tanzania leo Jumamosi kwa ziara ya siku moja ya kibinafsi ambapo atakutana na rais wa tanzania John Pombe Magufuli nyumbani kwake huko Chato.
Kulingana na taarifa iliotolewa na ikulu na kutiwa saini na mkurugenzi wa mawasiliano Gerson Msigwa viongozi hao wawili watafanya mkutano a faragha.
Ijapokuwa kuwa ni mkutano wa kuongeza udugu miongoni mwa viongozi hao ajenda ya mkutano huo unatarajiwa kuangazia maswala ya kibishara husuasana katika jamii ya Afrika mashariki.
Rais Museveni ni kiongozi wa pili kutoka kwa jamii ya Afrika mashariki kumtembelea rais Magufuli huko Chato wiki moja tu baada ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kuwasili nchini humo ili kumtembelea.
Vikwazo vya kibiashara
Katika mapokezi yake, Rais Uhuru Kenyatta alieleza furaha yake kujumuika na Watanzania na kumshukuru rais Magufuli kwa mualiko wake.
Alisema dhamira ya ziara hiyo ilikuwa kuimarisha uhusiano wa kijirani baina ya Kenya na Tanzania.
Alielezea umuhimu wa viongozi kuwajibika ili kuondosha vikwazo vinavyozuia biashara, kuruhusu mzunguko huru wa watu na kuzidi kuimarisha uhusiano na kusisitiza umuhimu wa mataifa ya Afrika mashariki kushikana kama kitu kimoja.
Kwa upande wake, mwenyeji rais John Magufuli alisisistiza lengo la taifa lake kuendelea kutunza uhusiano wa kieneo.
Rais Magufuli kwa sasa yuko katika likizo.
Museveni na Kagame kukutana?
Baadaye rais huyo wa Uganda anatarajiwa kukutana na rais wa Rwanda paul kagame jini Luanda Angola ambapo wanatarajia kuzungumzia kuhusu wasiwasi wa kisiasa uliopo kati ya mataifa hayo mawili.
Mgogo huo umezua hali ya wasiwasi katika mpaka a nchi hizo mbili huu pande zote mbili zikilaumiana.
Hivi majuzi rais wa Rwanda Paul Kagame alielezea kuwa chimbuko la mgogoro baina ya nchi yake na Uganda lianza miaka 20 iliyopita wakati majirani zake wa Uganda walipotaka kuangusha utawala wake.
Akihutubia mkutano huo wa kitaifa Rais Kagame alisema kwamba mgogoro huo ulishika kasi katika miaka ya hivi karibuni kutokana na serikali ya Uganda kuunga mkono kundi la RNC linalopinga Rwanda na ambalo linadaiwa kutumiwa na Uganda kuwanyanyasa raia wa Rwanda wanaotembelea au wanaoishi nchini Uganda.
Kwa upande wake Uganda imekuwa ikiishutumu Rwanda kuwatuma majasusi na kufanyia vitendo vya ujasusi kwenye ardhi yake, shutuma ambazo Rwanda inakanusha.
0 Comments