Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi wa Hifadhi, M. B. Moronda mara baada ya kufanya ziara ya kikazi katika Hifadhi ya Taifa Ibanda wilayani Kyerwa katika mwambao wa mto Kagera mpakani mwa Tanzania na Uganda. Katikati ni Kamishna Mwandamizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi , Martin Loibooki.
Wahifadhi wakiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu wilayani Karagwe wakati wa ziara ya Kikazi ya Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla katika hifadhi hiyo.
Na. Aron Msigwa – WMU
Serikali imesema itawapandikiza Sokwemtu katika hifadhi ya Taifa ya Rumanyika Orugundu iliyoko wilayani Karagwe na Ibanda iliyoko Kyerwa, mkoani Kagera kwa kuwa hifadhi hizo zina Ikolojia na chakula cha kutosha kinachoruhusu kustawi kwa wanyamapori hao hatua itakayochangia kukuza shughuli za utalii wa Sokwemtu hapa nchini na kuongeza pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ametoa kauli hiyo mkoani Kagera wakati wa ziara yake ya Kikazi ya kukagua maendeleo ya shughuli za uhifadhi katika hifadhi hizo zilizotangazwa hivi karibuni kuwa hifadhi za Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.
Dkt. Kigwangalla amesema mpango huo umekuja kufuatia taarifa za kitaalam zinaonesha kwamba katika miaka mingi iliyopita kulikua na Sokwemtu katika maeneo hayo ya wilaya ya Kyerwa na Karagwe ambayo watalaam wanasema ikolojia yake inaruhusu kustawi kwa wanyamapori hao kwa kuwa yana makazi mazuri na chakula cha kutosha.
Amesema mpango huo hautahusisha upandikizaji wa wanyamapori
0 Comments