Beyonce amefichua nyimbo zilizomo kwenye albamu yake mpya itakayoambatana na filamu mpya The Lion King remake na albamu hiyo imejumuisha wasanii nyota na wa juu wa muziki kutoka Afrika.
Wasanii wa Nigeria Tiwa Savage na Mr Eazi wanatumbuzia katika wimbo wa 'Keys to the Kingdom', wengine Tekno na Yemi Alade katika kibao 'Don't Jealous Me'.

Burna Boy ana kibao cha kipekee au solo, 'Ja Ara E', huku msanii wa Cameroon Salatiel akionekana akiimba na Beyonce na Pharrell Williams katika kibao 'Water'.
Wasanii wengine wa Afrika ni pamoja na Wizkid wa Nigeria, Shatta Wale wa Ghana, na Busiswa na Moonchild Sanelly kutoka Afrika kusini.
Alipotangaza mpango huo kwa mara aya kwanza wiki iliyopita, Beyonce alisema "Ilikuwa ni muhimu kuwa muziki usiimbwe na wasanii nyota na wenye vipaji bali iandaliwe na waandaaji wa Kiafrika. Ubora na moyo (mapenzi) vilikuwa vitu muhimu kwangu.
"Ni mchanganyiko wa kila kitu, si sauti moja tu. Kuna ushawishi kutoka kila kona, kutoka kwenye R&B, hip-hop na Afro Beat."
Tiwa savageHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMsanii nyota kutoka Nigeria Tiwa Savage pia ameshirikishwa pamoja na Mr. Eazi katika kibao 'Keys to the Kingdom'
Albamu hiyo ka jina 'The Lion King: The Gift', inatarajiwa kuzinduliwa Ijumaa hii.
Inajumuisha pia vibao vya ushirikiano na wasanii wa Marekani kama Kendrick Lamar, Pharrell Williams, Childish Gambino, na binti yake Beyonce, Blue Ivy miongoni mwa wengine.
Ni kibao tofauti kilichotumika kuisindikiza filamu hiyo ya The Lion King, Spirit, chenye mistari ya kiswahili, hatahivyo kimejumuishwa pia kwenye albamu hiyo.
Burna BoyHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBurna Boy
Wiki iliyopita, Beyonce aliachia kibao hicho kipya chenye maneno ya Kiswahili.
"Uishi kwa muda mrefu mfalme," sauti nyembamba inaimba kisha sauti nzito inaitika "uishi kwa", kionjo hiko kinajirudia mara mbili na kisha wimbo kuendelea kwa Kingereza.
Filamu mpya ya Lion King imetengenezwa na kampuni kubwa ya Disney nchini Marekani.