MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu ameamua kusaka vipaji vya waigizaji kwa njia ya usaili utakaofanyika Julai 27, 2019 katika Viwanja vya Leaders Club jijini Dar es Salaam ambao atawawezesha kupata fursa ya kushiriki kwenye tamthilia mbalimbali.
Usaili huo utakaofanyika saa 4 asubuhi hadi saa 10 jioni utahusu wanaume wenye kuanzia miaka 26 hadi 35, wanawake miaka 22-30, kinababa iaka 45-60 na kinamama miaka 45-60.