Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu sayansi na utamaduni, UNESCO limeutambua mji wa kale wa Babylon kuwa eneo la kihistoria.
Iraq imekuwa ikishinikiza tangu mwaka 1983 mji huo wa kale wa miaka 4,000-uijumuishwe katika orodha ya kifahari ya Umoja wa Mataifa.
Mji huo ulijulikana kwa bustani zake za kuning'inia, ambazo zilikuwa kati ya Maajabu Saba ya Dunia ya vitu vya kale duniani.
Miaka ya hivi karibuni eneo hilo limeharibiwa kufuatia ujenzi wa kasri la Saddam Hussein, na baadae kutumiwa kama kambi ya kijeshi kwa vikosi vya Marekani.
Kamati ya Urithi wa Dunia ya Umoja wa Mataifa ilikutana nchini Azerbaijan kuamua kuhusu maeneo mapya ya kale ambayo yanastahili kutambuliwa - ili yapewe tuzo kwa kuwa maeneo au nembo ya kihistoria inayozingatia muhimu binadamu wote na kulindwa na mikataba ya kimataifa..
Ujumbe wa Iraq ulikaribisha hatua hiyo, ukisema kuwa huu ni utambuzi wa mchango wa Babylon katika ustaarabu wa Mesopotamia.
Ikitangaza uamuzi huo, Unesco ilisema: "Hatua hii inaashiria utambuzi wa ubunifu wa hali ya juu ya mji wa-Babylon.
"Kuhusishwa kwa mji huo na moja ya maajabu saba ya vitu vya kale duniani.
Pia ilionya kuwa maeneo hayo yako katika "hali mbaya" na kwamba yanahitaji kuhifadhiwa haraka iwezekanavyo.
Ni maeneo yapi mapya ya kihistoria duniani?
Lisa Ackerman, afisa mkuu mtendaji wa muda wa Mfuko wa Dunia wa makumbusho, lenye makao yake New York- ameiambia BBC kuwa shirika hilo lisilokuwa la kiserekali limekuwa likifanya kazi na serikali ya Iran kwa miaka kuhifadhi uwanja wa Babylon.
Amesema sio "jambo la kawaida" kwa wanaharakati kushawishi kwa miongo kadhaa mji huo wa kale utambuliwe kama eneo la kihistoria duniani.
'Kuharibiwa vibaya'
Mwanzoni mwa miaka ya 1980, rais wa zamani wa Iraq Saddam Hussein aliharibu sehemu kubwa ya makaburi ya kihistoria na kujenga nyumba zingine zilizofanana na zile za zamani zilizokuwepo.
Baada ya vita vya ghuba, pia alijijengea kasri la kisasa upande wa pili la eneo hilo..
Mwaka 2005, Makavazi ya kitaifa ya Uingereza ilionya kuwa vikosi vya muungano vinavyoongozwa na Marekani vinasababisha uharibifu mkubwa katika mji huo wa kale.
John Curtis, ambaye ni mshirikishi wa makavazi hayo kitengo cha mashariki cha kati wakati huo, alionya katika ripoti yake kuwa magunia ya kubeba mchanga yamejazwa mabaki ya akiolojia ambayo inakadiriwa kuwa na miaka 2,600 na kubakisha mawe yaliyoharibiwa eneo hilo liliposhambuliwa.
Pia alipata ushahidi wa mafuta kuvuja katika mitaro ya inchi 12 ambayo ilichimbwa katika migodi ya madini hayo.
Ni sawa na "kujenga kambi ya kijeshi karibu na eneo hilo la kihistoria," alisema wakati huo.
Miaka minne baadae, Unesco ilisema kuwa "utumizi wa Babylon kama kambi ya kijeshi ni uvamizi mbaya wa eneo linalotambuliwa kimataifa kama eneo la vito vya kale.".
|
0 Comments