“Tumeamua kuimarisha kamati ya kitaifa ya kukabiliana na ugonjwa huu, ambayo sasa itakuwa chini ya Waziri Mkuu akisaidiwa na Waziri wa Afya, wajumbe wengine watachaguliwa na Waziri Mkuu kulingana na umuhimu wao.
“Kuanzia kesho Machi 23, 2020 wasafiri wote ikiwamo Watanzania watakaoingia nchini kutoka katika mataifa yaliyoathirika na Ugonjwa wa COVID-19 watafikia sehemu ya kujitenga kwa siku 14 na watakaa huko kwa gharama zao wenyewe.
“Naelekeza Wizara ya Afya na Mamlaka nyingine husika, kuhakikisha maabara yetu ya Taifa inaimarishwa kwa kupatiwa vifaa vya kisasa vya uchunguzi.
“Naagiza maeneo yote ya vituo vinavyotumiwa na watu kuingia nchini yapelekewe vifaa vya ukaguzi na pia kujikinga kwa ajili ya watumishi, vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe ulinzi wa mipaka yetu ili kuzuia watu kuingia bila uchunguzi.
0 Comments