MSIMAMIZI wa uchaguzi Jimbo la Iringa Mjini amemtangaza mgombea ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jesca Msambatavangu,  kuwa mshindi wa ubunge wa jimbo hilo kwa kupata kura 36,034 dhidi ya mpinzani wake, Peter Msigwa, wa Chama cha Demokrasia na Mandeleo  (Chadema) aliyepata kura 19,331. Msigwa alikuwa akilitetea jimbo hilo aliloliongoza kwa miaka 10.