Taswiara ya eneo la Jangwani kama linavyoonekana kufuatia mafuriko ambayo yametokea eneo la Jangwani na kusababisha barabara hiyo kufungwa.

Baadhi ya wananchi wakipita kwa tabu eneo la Jangwani.

Makazi yaliyopo eneo ya Jangwani kama inavyoonekana.

Daladala lililokuwa likitokea maeneo ya kariakoo likionekana kuzama maji eneo la Jangwani.

Baadhi ya wananchi wakilazimisha kupita katikati ya mafuriko. 

Baadhi ya wananchi wanaofanya shughuli zao katika maeneo ya Kariakoo na Posta wameshangazwa na mafuriko ambayo yametokea mchana wa leo katika eneo la Jangwani baada ya kufurika mto msimbaza na kusababisha barabara hiyo ya morogoro kufungwa.

 

Mtandao huu umefanikiwa kufika eneo hilo na kushuhudia mafuriko hayo ambapo baadhi ya wananchi wameonekana kupita katikati ya mafuriko hayo huku usafiri wa daladala na magari mengine yakishindwa kupita.

 

Baadhi ya wananchi waliozungumza na mtandao huu wamesema kuwa wameshangazwa kutokea kwa mafuriko hayo kwani katika jiji la Dar es Salaam hakuna mvua ambayo imenyesha kwa takribani siku kama tatu hivi huku wakieleza kuwa huenda mafuriko hayo yamesababishwa na mvua zilizonyesha maeneo ya Chanika na Kisarawe mkoa wa Pwani kwani maji yanayotoka maeneo hayo yanatiririsha mto msimbazi.

 

Moja ya daladala lililokuwa likitokea maeneo ya kariakoo lilionekana likiwa limezimika katikati ya mafuriko eneo hilo la Jangwani ambapo baadhi ya mashuhuda wamesema abiria waliokuwemo wamelazimika kuvushwa kwa usafiri wa baiskeli aina ya ‘Guta’.