Maalim Seif

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Maalim Seif na viongozi wengine wa chama hicho wamekatwa visiwani Zanzibar.

Kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amethibitisha kukamatwa kwa Maalim Seif pamoja na viongozi wengine akiwemo Makamu Mwenyekiti Juma Duni Haji na Mjumbe wa Kamati Kuu.

Ruka Twitter ujumbe, 1

Mwisho wa Twitter ujumbe, 1

Maalim Seif alikamatwa muda mfupi baada ya kutangaza kuongoza maandamano ya amani ili kutetea haki yao ya kidemokrasia.

Siku ya Jumanne Maalim Seif alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha mtoni Garagara na na kupelekwa makao makuu ya polisi kisiwani Zanzibar ambako aliachiliwa saa kadhaa baadaye katika hatua ambayo ilishutumiwa vikali na viongozi wa upinzani.

Maalim Seif ni nani?

Seif Sharif Hamad alizaliwa Mtambwe, kisiwani Pemba, Zanzibar, Oktoba 1943. Alisoma elimu yake ya msingi na upili katika visiwa hivyo kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kusomea shahada ya kwanza ya Sayansi ya Siasa.

Huyu ni mwanasiasa aliyehudumu katika nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali ya mapinduzi tangu akiwa CCM hadi CUF.

Kabla ya kuwa mwanasiasa alikuwa Mwalimu aliyesomesha shule kadhaa Unguja na Pemba.

Kuna kila dalili ya kuwa safari yake ya kisiasa itahitimika akiwa katika chama chake kipya.

Kitendawili kilichobaki ni ikiwa itahitimika kwa kufanikiwa zile ndoto za muda mrefu za kuwa Rais ama itahitimika kwa kuwa simba wa kisiasa aliyepambana na hatimae akamalizika bila lengo kuu kutimia.

Historia ya uchaguzi Zanzibar

Kisiwa hicho kina historia ya uchaguzi unaogombaniwa. Uchaguzi wa mwaka 2005 ulizongwa na ghasia.

Uchaguzi wa mwisho wa 2015 ulifutiliwa mbali na mkuu wa tume ya uchaguzi kwa kutokuwa huru na haki.

Upinzani ulisusia marudio ya Uchaguzi huo na mgombea wa CCM akatawazwa mshindi.

Kuna wagombea 17 wanaowania wadhfa wa urasi kisiwani Zanzibar.

Hatahivyo ushindani mkali ni ule uliopo kati ya kiongozi wa upinzani Maalim Seif Sharrif Hamad ambaye anawania kwa mara ya sita dhidi ya Hussein Mwinyi, mwana wa aliyekuwa rais wa zamani wa taifa hilo.

Rais Ali Mohammed Shein anaondoka baada ya kuhudumu kwa mihula miwili.