Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda (kulia) akizindua jengo la choo cha wasichana sekondari ya Kilimamoja Iliopo Wilayani Karatu mkoani Arusha  (picha na Woinde SHIZZA,Arusha)

Mkuu wa wilaya ya Karatu  Abbas Kayanda akikagua jengo la choo cha wasichana sekondari ya Kilimamoja juzi iliojegwa na Wafadhili wa Africa foundation (picha na Woinde SHIZZA,Arusha).



Wafadhili wa Africa foundation wamekabidhi kwa serikali ujenzi wa bweni la wavulana na jengo la choo cha wasichana vyenye thamani ya shilingi million 113 kwa shule ya sekondari kilimamoja. 

Bweni la wavulana lina uwezo wa kubeba wanafunzi 64 litakuwa msaada kwa wanafunzi wanaotoka mbali na eneo la shule.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Abbas Kayanda amewapongeza wafadhili hao kwa msaada waliotoa kwa shule ya sekondari kilimamoja ,nakusema wadau wa elimu kazi wanayofanya ni kuunga mkono kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuimarisha miundo mbinu katika shule ya msingi na sekondari. 

Alisema serikali imetengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na mambo haya wanayoyafanya wawekezaji hawa ni kurudisha shukrani kwa jamii.

Kayanda alisema muwekezaji Africa foundation anaamini kabisa njia pekee ya kuikomboa jamii ni kuwekeza katika elimu,na elimu inatoa maarifa ambayo yakiingia kichwani hayawezi kupotea. 

Aliwaasa wanafunzi kusoma kwa bidii ili elimu yao ije kusaidia jamii, ammbapo alifafanua kuwa ili mwanafunzi aweze kufikia malengo yake lazima awe na nidhamu,Lazima miundo mbinu iliyojengwa ichochee kiwango cha ufaulu wa wanafunzi ,na mabadiliko ya kitaaluma ndio yatakayoonyesha umuhimu wa miundo iliyojengwa.

Aidha alitoa wito kwa walimu kusimamia na kuhakikisha miundo mbinu inadumu kwa muda mrefu, lakini kuchukua hatua stahiki kwa mtu yeyote atakayeharibu miundo mbinu, na kuwaasa wanafunzi kuwa na nidhamu ya matumizi ya miundo mbinu iliyojengwa na kila mwanafunzi kuwa mlinzi wa mwenzake.

Awali Afisa elimu sekondari Kalista Maina alisema bweni lilojengwa litasaidia wanafunzi kupunguza utoro wa mara kwa mara na vishawishi mbalimbali,nakubainisha kuwa bweni hilo litawaongezea umakini wa kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza malengo yao. 

Alisema bweni litasaidia wanafunzi kupata muda mwingi wa kujisomea wakati wa usiku lakini kuwaondolea wanafunzi uchovu wa kutembea umbali mrefu kutoka nyumbani,Ambapo aliwaomba wazazi kuwajibika kwa watoto wao kwa kuhakikisha wanapatia wanafunzi mahitaji yote muhimu kwa wakati.

Naye Mkurugenzi wa Africa Foundation Dkt. Ernest Mgono alisema shule ya sekondari kilimamoja ipo karibu na maeneo ya hifadhi na maeneo hayo ya hifadhi, katika maeneo hayo ya uhifadhi ndipo walipoweka vitega uchumi vyao, hivyo kwa kuwa katika maeneo waliyowekeza kuna jamii inawazunguka lazima jamii ipate faida kidogo ili waendelee kujali na kutunza hifadhi.

Dkt. Mgono alisema walishaanza kujenga bwalo la chakula lakini wameshajenga bwalo la wanafunzi wa kike kabla ya kukabidhi bwalo la wanafunzi wa kiume ,Aliwaomba wanafunzi kutunza majengo yote yaliyojengwa ili majengo hayo yaweze kudumu kwa muda mrefu.