Uteuzi wa Waziri wa zamani wa biashara wa Nigeria kuongoza Shirika la Biashara Duniani (WTO) umekumbwa na utata baada ya Marekani kupinga hatua hiyo.
Siku ya Jumatano, kamati ya uteuzi ya WTO ilipendekeza wanachama 164 wamteue Ngozi Okonjo-Iweala.
Atakuwa mwanamke wa kwanza na Mwafrika wa kwanza kuongoza WTO.
Lakini Marekani, ambayo imekuwa ikikosoa jinsi WTO inavyoshughulikia biashara ya kimataifa, inamtaka mwanamke mwingine Yoo Myung-hee, kutoka Korea Kusini ikisema huenda akabadilisha shirika hilo.
Ms Okonjo-Iweala alisema nimekubali kuteuliwa kwa "unyenyekevu mkubwa".
Lakini mchakato huo wa uteuzi wa miezi minne wa kumtafuta Mkurugenzi mkuu wa WTO umegonga mwamba baada ya Washington kusema itaendelea kumuunga mkono waziri wa biashara wa Korea Kusini.
Katika taarifa iliyokosoa WTO, ofisi ya mwakilishi wa biashara ya Marekani, ambayo humshauri Rais Donald Trump kuhusu sera za biashara, ilisema shirika hilo "lazima liongozwe na mtu wa kisawa sawa aliye na uwezo na tajiriba katika nyanja hiyo".
Bi Yoo alikuwa "amejinadi" kama mtaalamu wa masuala ya biashara aliye na "ujuzi wote muhimu unaohitajika kuongoza shirika hilo", taarifa hiyo ilisema.
Iliongeza: "Huu ni wakati mgumu sana kwa WTO NA biashara ya kimataifa . Hakujakuwa na majadiliano kuhusu masuala ya ushuru kwa miaka 25, mfumo wa kusuluhisha mizozo umesambaratika, na wanachama wachache sana hutimiza majukumu yao ya uwazi. WTO inahitaji mageuzi makubwa ."
Taarifa hiyo haikumtaja Bi Okonjo-Iweala.
Mapema Jumatano, baada ya wajumbe wa WTO kukutana kujadili uteuzi wake, msemaji Keith Rockwell alisema ni taifa moja lenye mwanachama pekee ambaye haimuungi mkono Bi Okonjo-Iweala.
"Wajumbe wote ambao walitoa maoni yao leo wameonesha kuunga mkono…. matakeo ya mchakato huu isipokuwa mmoja," alisema.
'Shughuli nyingi'
Bw. Trump ameitaja WTO kama shirika la "kutisha" na ambalo linapendelea China, na kwamba baadhi ya uteuzi wa nyadhifa muhimu katika shirika hilo tayari zimepingwa.
Shirika la WTO limeitisha mkutano Novemba tarehe 9 - baadaye ya uchaguzi wa Iraqis wa Marekani - kujadili suala hilo.
Hatua ya Marekani kupinga haimanishi raia huyo wa Nigeria hatateuliwa, hata hivyo Washington huenda ikawa na ushawishi mkubwa katika uamuzi wa mwisho.
Bw. Rockwell aliwaambia wanahabari kwamba huenda kukawa na "shughuli nyingi" za kutafuta makubaliano ya uteuzi wa Bi Okonjo-Iweala ambaye pia anaungwa mkono na Muungano wa Ulaya.
Mzozo wa uongozi ulisababishwa na mkuu wa WTO anayeondoka Roberto Azevedo kujiuzulu mwaka mmoja kabla ya muda wake kuisha. WTO kwa sasa inaongozwa na manaibu wanne.
Bi Okonjo-Iweala, 66, amehudumu kama waziri wa kwanza wa kike wa fedha na mambo ya nje wa nchi yake na amefanya kazi na Benki 25.
Pia anahudumu kama mkurugenzi wa bodi ya usimamizi wa Twitter, mwenyekiti wa muungano chanjo wa GAVI na jumble malum wa Shirika la Afya Duniani(WHO)katika mapambano dhidi ya Covid-19.
Ikiwa Bi Okonjo-Iweala hatimaye atateuliwa kuongoza shirika hilo atakutana na majukumu change nzima. WTO tayari inakabiliwa na changamoto ya kukwama kwa mazungumzo ya kibiashara na uhasama kati ya Marekani na China.
Mapema mwezi huu alisema tajiriba yake kubwa ya muleta mageuzi imemfanya kuwa mtu sahihi atakayesaidia WTO kurejea ulingozi. "Mimi ni mgombea wa mageuzi na nadhani WTO sasa inahitaji hati na maarifa ya mageuzi.
0 Comments