Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Musa (kulia) akiwa pamoja na Sheikh Muhammad Idd.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Alhad Musa, pamoja na Sheikh Muhammad Idd, wamekutana na kuzungumza na kusameheana baada ya kurushiana maneno siku chache zilizopita.

 

Kwa pamoja wamewaomba wananchi na waumini wa Kiislamu kutohusisha ugomvi wao na mamabo ya siasa na kusisitiza kuwa kwa yaliyotokea ni mapungufu yao ya kibinadamu na wala isichukuliwe kama ni waislamu wote ndio wenye tabia hiyo.