Tetemeko la Ardhi lililotokea mchana wa Ijumaa ya tarehe 30 Octoba 2020 katika ukanda wa Bahari ya Aegean limeharibu miundombinu katika miji ya pwani.

Watu katika Mji uliopo Magharibi mwa Uturuki , Izmir wamekusanyika katika mitaa baada ya kuyakimbia majengo yao wakitafuta usalama. Meya wa mji wa Izmir amethibitisha kuwa takribani majengo 20 yameharibiwa katika Mji huo.

Taarifa zilizotolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani Suleyman Soylu kupitia mtandao wa Twitter ni kuwa Miji mingine iliyoharibiwa na Tetemeko hilo ni Bornova, Bayrakli.

Aidha Waziri Soylu ameongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea katika eneo hilo. Taarifa zaidi zinaeleza kuwa takribani watu wanne (4) wamefariki huku 120 wakiwa wamejeruhiwa kufuatia Tetemeko hilo.