MFALME wa masauti BongoChristian Bella ametoboa siri yake mwanamama Hamisa Mobeto. Bella amekiambia CHANZO kuwa, wazo la kuimba na Mobeto alilipata nchini Marekani walipokuwa wamekwenda pamoja.

 

Bella anasema kuwa, Mobeto anafanya vizuri pale anapokuwa anaelekezwa ila kuhusiana na kuimba, bado anahitaji mazoezi makubwa mno.

 

“Hamisa (Mobeto) siyo muimbaji mkali; yaani yule wa kusema ndiye bora au levo za juu kabisakabisa, lakini ni mtu ambaye ana kichwa chepesi, ukimuelekeza anajua haraka sana, tofauti na wasanii wengine,” anasema Bella ambaye ni Mkurugenzi wa Bendi ya Malaika.

 

Ikumbukwe kwamba, mwaka jana, wawili hao waliachia wimbo wa pamoja unaokwenda kwa jina la Boss na ulipata mapokezi mazuri kwa mashabiki wao.