Wakili wa Bi Macron alithibitisha kuwa atachukua hatua kuhusu madai hayo ghushi

Brigitte Macron anatazamiwa kuchukua hatua za kisheria kuhusu madai ya mtandao kwamba yeye ni mwanamke aliyebadili jinsia na alizaliwa akiwa mwanaume.

Mke wa rais wa Ufaransa amelengwa kwenye mitandao ya kijamii kwa madai hayo ya uwongo, baada ya kuchapishwa kwenye tovuti ya mrengo wa kulia mnamo Septemba na kusambazwa na wananadharia wa njama.

Uvumi huo unadai alizaliwa akiwa mwanaume kwa jina Jean-Michel Trogneux.

Jina limevuma kwenye mitandao ya kijamii na kutajwa makumi ya maelfu.

Wakili wa Bi Macron - ambaye ni mama wa watoto watatu wazima kutoka kwa ndoa yake ya kwanza - alithibitisha kuwa anachukua hatua.

"Ameamua kuanzisha kesi, inaendelea," wakili Jean Ennochi alithibitisha kwa shirika la habari la AFP.

Uwongo kumhusu Brigitte mwenye umri wa miaka 68 umeenezwa na akaunti zinazompinga mumewe, Rais Emmanuel Macron, zikiwemo zile za siasa kali za mrengo wa kulia, vikundi vya kupinga chanjo na vuguvugu la njama la QAnon.

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimefuatilia hadithi hiyo hadi makala iliyoandikwa kwenye jarida la mrengo mkali wa kulia na mwanamke anayeitwa Natacha Rey. Kisha ikapata watazamaji wengi zaidi baada ya kujadiliwa katika tangazo lililotazamwa sana la YouTube na mitazamo iliyoshirikiwa mtandaoni na watu mbalimbali wanaopinga chanjo na wanaharakati wa mrengo mkali wa kulia, kulingana na gazeti la Libération.

2px presentational grey line

Jibu la kisheria kwa dai la kipuuzi

Uchambuzi na Hugh Schofield, Mwandishi Paris

Kile ambacho watu wengi wanauliza ni kwa nini Brigitte Macron anaenda kortini kuzuia uzushi wa kipuuzi sana. Je! Jamaa wa Elvis waliwasilisha kesi walipoambiwa kwamba yuko hai na yuko mzima, baada ya kuonekana akila nyama ya nguruwe na huko Memphis?

Kufungua kesi mbele ya mahakama kunaweza kutoa hisia kwa wenye kuamini hayo kwamba kweli kuna jambo la kukandamiza. Vinginevyo, kwa nini wangeichukua kwa uzito hivyo?

Lakini kwa kweli hakuna ushahidi kwamba mtu yeyote - zaidi ya wachache wajinga - anachukulia hadithi ya Brigitte kuwa mtu aliyebadili jinsia kuwa ya kweli

Wanahabari na wanamitandao kwa pamoja wanaweza kusisitiza umuhimu wa trafiki ya mtandao. Kwa hivyo hadithi ilipata kusomwa kwa wingi , hiyo haimaanishi kuwa kuna mtu aliamini.

Na kama Le Monde ilivyosema, wananadharia wa njama wa Ufaransa wana samaki wengine wa kukaanga. Kwa sasa wanahangaikia uchaguzi unaokaribia, na jinsi unavyoweza au kutoweza kuibiwa na mamlaka .

Kwa waumini wa QAnon, hadithi ya Brigitte ni ya kukengeusha sana, mbaya zaidi ni mmea usioaminika hivi kwamba dhumuni lake halisi linaweza kuwa tu kuwadharau. Aha! Nadharia nyingine ya njama!

2px presentational grey line

Hii si mara ya kwanza kwa Bi Macron kulengwa tangu mumewe achaguliwe mwaka wa 2017, kwani kejeli za mtandaoni hapo awali zililenga pengo la umri kati ya wanandoa hao la karibu miaka 25.

Brigitte Macron (C) and her daughters Tiphaine Auziere (R) and Laurence Auziere-Jourdan (L) attend a campaign event on April 17, 2017 at the Bercy Arena in Paris.

CHANZO CHA PICHA,ERIC FEFERBERG/AFP

Maelezo ya picha,

Brigitte Macron alikuwa na binti zake wawili kando yake kwenye hafla ya kampeni mnamo 2017

Nadharia ya njama hiyo inakuja wakati Ufaransa inakabiliwa na uchaguzi wa urais mnamo mwaka wa 2022.

Bw Macron bado hajathibitisha rasmi kuwa atawania muhula wa pili lakini anatarajiwa na wengi kufanya hivyo.

Anakabiliwa na ushindani kutoka kwa Valérie Pécresse, mgombea wa chama cha mrengo wa kulia cha Republicans, na Eric Zemmour, mtangazaji wa TV wa Ufaransa na mwandishi, ambaye anatarajia kuwakilisha chama cha mrengo mkali wa kulia.