Umoja wa Falme za Kiarabu,UAE umetangaza kutasitisha safari za ndege kwa abiria kutoka Tanzania Kenya, Ethiopia, na Nigeria na kuongeza vikwazo vya usafiri kwa ndege za Uganda na Ghana, kuanzia Desemba 25.
Mamlaka ya Kitaifa ya Kudhibiti Dharura na Majanga (NCEMA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (GCAA) wa nchi hiyo zimesema hatua hizo mpya zitaanza kutekelezwa kwanzia saa moja na nusu usiku wa Jumamosi.
Hatua hiyo inajumuisha kusimamisha kuingia nchini humo kwa wasafiri waliokuwa katika nchi hizo nne siku 14 kabla ya kusairi UAE. Hata hivyo safari za ndege kutoka UAE hadi nchi hizo zinaendelea kama zilivyoratibiwa.
Nchi hiyo pia imeweka masharti mapya ya usafiri kwa abiria wanaokuja kwa ndege za moja kwa moja kutoka Uganda na Ghana.
Masharti hayo ni pamoja na kufanyiwa vipimo vya cha COVID-19 ndani ya saa 48 na na kufanyiwa vipimo vya-PCR kwenye uwanja wa ndege ndani ya saa sita kabla ya kuanza safari.
Raia wa UAE wamezuiwa kusafiri kwenda nchi hizo nne za Kiafrika isipokuwa kwa matibabu ya dharura, ujumbe rasmi na ufadhili wa masomo.
Wale walioondolewa kwenye marufuku ya usafiri lazima wawasilishe vipimo hasi vya PCR ndani ya saa 48 baada ya muda wao wa kuondoka, wakapime haraka PCR kwenye uwanja wa ndege saa sita kabla ya kuondoka, na mwafanyiwe tena vipimo watakapowasili UAE.
Hivi karibu Tanzania ilizindua mashine nyingine kubwa na ya kisasa kwa ajili ya kupima kipimo cha haraka cha Covid -19 kwa wasafiri wanaoenda nchi za Falme za Kiarabu, baada ya nchi hiyo kuwataka wasafiri wanaotokea Tanzania kwenda Dubai, kupata vipimo vya masaa 48 na kisha kumalizia na kipimo cha saa sita kabla ya safari.
0 Comments