Margarita Gracheva

"Alinipeleka msituni, mahali pweke. Na akanipigia kelele: 'Weka mikono yako juu ya mti!'" "Nililia, nikapiga kelele na kumsihi asinidhuru."

"Aliniambia nisitazame akaanza kunikata mikono." Hii ni hadithi ya Mrusi Margarita Gracheva mwenye umri wa miaka 26, mwathirika wa unyanyasaji wa mumewe.

Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu imekubaliana naye hivi punde, ikitoa uamuzi kwamba serikali ya Urusi lazima imlipe fidia ya dola za Marekani 400,000 kwa ajili ya sheria legevu kuhusu unyanyasaji wa majumbani nchini humo.

Mnamo mwezi Desemba 2017, baada ya kuacha watoto kwenye shuleni, mume wa zamani wa Margarita Dmitry Grachev alimpeleka msituni nje ya Moscow.

Huko alitengeneza michoro kwenye mikono yake na kukata mikono yake yote miwili kwa shoka.

Las manos de Margarita Gracheva.

Baada ya hapo, alimpeleka hospitalini akivuja damu na kuwapa madaktari sanduku lililokuwa na mkono wa kulia wa mke wake. Kisha akajisalimisha kwa polisi.

Kesi ya Margarita iliangazia jinsi sheria za Urusi kuhusu unyanyasaji wa nyumbani zilivyolegea, baada ya makosa kadhaa kuondolewa katika kanuni za uhalifu mwaka wa 2017 chini ya serikali ya Vladimir Putin.

Mume wake wa zamani alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.

Vitisho

Mwezi mmoja kabla ya Margarita kushambuliwa kwa shoka, mumewe alikuwa amemtishia kwa kisu. "Alichukua kisu na kukiweka kooni mwangu.

Na aliendelea kurudia: 'Kubali! Je, unanidanganya au la?" Margarita aliiambia BBC mwaka wa 2018.

"Nilipokwenda polisi nilikuwa na uhakika wangekuja siku iliyofuata na kufanya jambo. Lakini hawakufanya hivyo."

"Polisi aliniambia: "Wewe na yeye mtapatana. Hili sio muhimu." Mwanzoni mwa Desemba, kesi ilifungwa. Siku tatu baadaye, alinipeleka msituni na kunikata mikono," alisema.

Dmitry Grachev.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Sheria

Mnamo Februari 2017, Bunge la Urusi liliondoa baadhi ya sheria za kanuni za uhalifu zinazoadhibu unyanyasaji wa nyumbani.

Mashambulio ya kwanza ambayo mwathiriwa hafikii hatua ya kulazwa hospitalini hayachukuliwi tena kama makosa ya jinai na adhabu zilipunguzwa.

Uamuzi huu ulisababisha maandamano kadhaa ya wanaharakati katika mitaa ya Urusi.

Ripoti ya shirika la Human Rights Watch (HRW) ilionya kuwa mabadiliko ya sheria yanawanyima wanawake ulinzi muhimu.

Serikali ya Urusi ilitupilia mbali ripoti ya HRW ikisema kuwa mahojiano mengi hayawakilishi ukweli.

Katika kisa cha Margarita, sawa na wanawake wengine wengi nchini Urusi, kuteswa kimwili kulianza mume wake alipoanza kumpiga.

Margarita Gracheva con periodistas tras la lectura de la sentencia contra su exesposo.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mara ya kwanza "Nilifikiri kitu cha ajabu kilikuwa kinatokea.

Ilikamilika tu kama kesi ya utawala na sio uhalifu.

Unampiga mtu na unaadhibiwa kwa faini tu." "Kwa upande wangu, alitozwa faini ya rubles 10,000 (dola za Marekani 150)," alielezea.

Margarita Gracheva in hospital

CHANZO CHA PICHA,MARGARITA GRACHEVA

Hukumu

Dmitry Grachev.

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Mume wa zamani wa Margarita alishtakiwa kwa utekaji nyara, kutishia kumuua na kumjeruhi mke wake vibaya. Katika mchakato wa mahakama, alikiri kukata mikono ya Margarita.

Mwanaume huyo alihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela.

Watoto wake wawili pia walizuiwa kumuona. "Watoto wangu hawajui kilichotokea. Wanafikiri nimepata ajali. Ni vigumu kwao. Sijui nitawaelezaje," alisema Margarita.

"Kwangu mimi, jambo bora zaidi lingekuwa kama wangempa kifungo cha maisha jela. Hilo lingeniweka salama. Ikiwa hatimaye ataishi karibu, hiyo haitakuwa salama kwangu au kwa watoto." "Mkono wangu wa kushoto ulipotea msituni. Waliupata baadaye.

Margarita Gracheva

Ulikuwa umevunjwa mifupa katika sehemu nane.

Nilipandikizwa ngozi na mishipa," alisema Margarita.

Madaktari walishona mkono wake wa kushoto katika operesheni iliyochukua takriban saa 10.

Watu kutoka kote ulimwenguni walituma michango ambayo ilifikia $ 65,000 ili mwanamke huyo apate mkono wa kulia wa bionic.