TANZANIA ASSOCIATION { VZW }
Tanzania Association iliyopo nchini Ubelgiji inapenda kuwatangazia watanzania wote kwamba siku ya Jumamosi ya tarehe 05/02/2022 katika jiji la Antwerpen kutafanyika mkutano mkubwa wa watanzania.
Mahala pa kukutania ni ukumbi unaoitwa OUD BADHUIS na anuani ya kufika ukumbini hapo ni kama ifuatavyo,
ALFONS ANGELSSTRAAT 16
2060-ANTWERPEN
MUDA NI SAA 9 ALASIRI {15hrs} Tunakuomba kwa mapenzi na nchi yako ujumuike nasi kwani kuna mengi hutakiwi kuyakosa.
Kufika kwako kutafanikisha kikao chetu kile kizuri zaidi na tunakuomba umtaarifu kila mtanzania unayemfahamu.
Tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwako.
0 Comments