TIMU ya Taifa ya Senegal imekumbwa na janga la wachezaji watatu kukutwa na virusi vya Corona pamoja na viongozi wao wengine sita waliokuwa kwenye msafara huo wa kujiandaa kwenda Cameroon kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).

 

Wachezaji hao ni Nampalys Mendy wa Leicester City, Pape Sarr anayekipiga kwa mkopo Metz akitokea Tottenham na Mame Thiam wa Kayseripor.

 

Hiyo imekuwa taarifa mbaya zaidi kwa Senegal, baada ya awali kuelezwa kuwa wanaweza kumkosa nyota wao, Ismaila Sarr anayekipiga Watford kutokana na majeraha aliyonayo.

 

Senegal inatarajiwa kuanza mchezo wake wa kwanza Januari 10 dhidi ya Zimbabwe kabla ya kukutana na Guinea na Malawi kwa ajili ya kukamilisha mechi zao za Kundi B.