KASRI  la Buckingham limethibitisha kuwa Malkia wa Uingereza Elizabeth II amebainika kuugua ugonjwa wa  Covid- 19  leo Februari 20, 222

Malkia huyo amepata baadhi ya dalili za Covid 19 ikiwemo kupata baridi kali na ataendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa Madaktari na kufuata miongozo ya Covid 19 ikiwemo kujitenga.

 

Naye Waziri Mkuu Boris Johnson  kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter  amesema anamuombea Malkia aweze kupona haraka huku akitoa wito kwa Waingereza kumuombea Malkia kupona haraka.