Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan, pichani akizungumza na Watanzania waishio Ughaibuni siku ya ijumaa ya tarehe 18.02.2022 katika ukumbi wa La Plaza Hotel uliopo jijini Brussel nchini Ubelgiji.Rais Samia pia alishiriki chakula cha jioni na watanzania hao na kuwasihi kuishi kwa amani na upendo nchi za watu.

{Picha zote na Maganga One Blog}


Pichani ni baadhi ya kina mama wenye kikundi cha Upendo Group kilicho jijini Brussel nchini Ubelgiji ambacho kimekuwa kikijikita zaidi katika utoaji wa misaada nchini Tanzania.Kikundi cha Upendo kilitoa shukrani za dhati kwa ujio wa Mhe:Rais Samia na kuahidi kusaidia zaidi nyumbani Tanzania.Rais alikutana na Watanzania hao waishio Ughaibuni katika ukumbi wa La Plaza Hotel siku ya Ijumaa tarehe 18.02.2022 jijini Brussel nchini Ubelgiji
{Picha na maelezo kutoka Maganga One Blog}
Waziri wa Fedha Mhe: Mwigulu Nchemba akimkaribisha Rais wa Jamuhui ya Muungano wa Tanzania Mhe: Samia Suluhu Hassan katika ukumbi wa La Plaza Hotel uliopo jijini Brussel nchini Ubelgiji siku ya Ijumaa ya tarehe 18.02.2022.Rais Samia alikutana na Watanzania waishio Ughaibuni katika chakula cha jioni kilichoandaliwa na wana Diaspora wa Belux.{Picha zote na maelezo kutoka Maganga One Blog}

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan{Pichani katikati} akijibu baadhi ya maswali siku ya ijumaa  ya tarehe 18.02.2022 katika ukumbi wa La Hotel Plaza jijini Brussel nchini Ubelgiji aliyokuwa akiulizwa na baadhi ya Watanzania waishio Ughaibuni kuhusu masuala yanayohusu maendeleo ya nchi kwa ujumla.Pichani kulia ni Waziri wa Fedha nchini Tanzania Mhe:Mwigulu Nchemba ambaye aliambatana na Mhe:Rais katika ziara ya kikazi Barani UlayaKulia kwa Mhe: Waziri Nchemba ni Mwenyekiti wa Diaspora Ubelgiji ndugu Gaspar Ndabi,kulia kwa Mhe:Rais ni Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe;Jestas Abouk Nyamanga na mwisho kabisaa ni Mwenyekiti wa Watanzania Diaspora anayeiwakilisha Luxembourg ndugu,Mwaruka Mgaya.{Picha zote na maelezo kutoka Maganga One Blog}

Afisa Balozi waa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe:Juma Salum akiingia ukumbi wa La Hotel Plaza siku ya ijumaa tarehe 18.02.2022 katika makutano ya  Watanzania waishio Ughaibuni na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Samia Suluhu Hassan jijini Brussel nchini Ubelgiji.

Pichani kushoto ni Mwenyekiti wa Tanzania Chamber of Commerce,Industry & Agriculture Mr.Paul Koyi na mmoja wa viongozi wa Diaspora nchini Ubelgiji ndugu Jamil Saleh wakifuatilia kwa karibu hotba ya Mhe:Rais Samia Suluhu Hassan siku ya ijumaa tarehe 18.02.2022 katika ukumbi wa La Hotel Plaza jijini Ubelgiji

Mmoja wa Mtanzania aishie nchini Luxembourg ndugu Nassir  alipata nafasi kuuliza swali kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan siku ya ijumaa ya tarehe 18.02.2022 katika ukumbi wa  LaHotel Plaza uliopo jijini Brussel nchini Ubelgiji.{Picha zote na maelezo kutoka Maganga One Blog}
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe:Samia Suluhu Hassan akipata picha na Watanzania waishio Ughaibuni siku ya ijumaa ya tarehe 18.02.2022 katika ukumbu wa Plaza hotel jijini Brussel ambapo Mhe:Rais alikutana na watanzania katika chakula cha jioni,Mhe:Rais aliambana na viongozi mbalimbali wa Serikali katika ziara yake barani Ulaya.

{Picha zote na maelezo kutoka Maganga One Blog}