Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amemtembelea na kuzungumza na Mjane wa aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano hayati Dkt. John Magufuli, Mama Janeth Magufuli nyumbani kwake Wilayani Chato Mkoani Geita leo Machi 16, 2022. 

Spika Dkt. Tulia pia ametembelea kaburi la hayati Magufuli pamoja na kusaini kitabu cha kumbukumbu.