Nchi za Magharibi zilikataa matokeo ya uchaguzi wa Urusi. Josep Borrell, mkuu wa masuala ya kigeni wa Umoja wa Ulaya, alisema kwa niaba ya shirika hilo kwamba uchaguzi ulifanyika chini ya shinikizo la utaratibu.

Nchi kadhaa za Umoja wa Ulaya zikiwemo Ufaransa na Ujerumani zimesema moja kwa moja kwamba hazitampongeza Rais Putin.

Hatahivyo Beijing ilimpongeza Putin mapema.

Rais Xi Jinping wa China alisema kuwa matokeo ya uchaguzi huo yanaonyesha kikamilifu uungaji mkono wa watu wa Russia. Marais wa Iran na Belarus walielezea ushindi wa Putin kuwa wa maamuzi na wa kuvutia mtawalia.