Mawimbi mabaya ya joto katika Afrika Magharibi na Sahel hayawezi kuisha bila mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababishwa na binadamu, wanasayansi wanasema.

Halijoto imeongezeka na kufikia zaidi ya nyuzijoto 48C nchini Mali mwezi uliopita huku hospitali moja ikihusisha mamia ya vifo na joto kali.

Watafiti wanasema shughuli za binadamu kama vile kuchoma mafuta zilisababisha ongezeko la nyuzijoto 1.4C na kuwa ya joto zaidi zaidi kuliko kawaida.

Utafiti tofauti kuhusu ukame Kusini mwa Afŕika ulionyesha kuwa El Niño ndio ya kulaumiwa, badala ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Nchi kadhaa katika eneo la Sahel na Afrika Magharibi zilikumbwa na wimbi kali la joto lililopiga mwishoni mwa Machi na kudumu hadi mapema Aprili.

Joto hilo lilikuwa la hali ya juu zaidi katika mikoa ya kusini ya Mali na Burkina Faso.

Mjini Bamako, mji mkuu wa Mali, Hospitali ya Gabriel Toure ilisema ilirekodi vifo 102 katika siku za kwanza za mwezi Aprili.

Karibu nusu ya watu waliokufa walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, na hospitali ilisema kuwa joto lilichangiavingi ya vifo hivyo.

Watafiti wanaamini kuwa mabadiliko ya hali ya hewa duniani yalikuwa na jukumu muhimu katika wimbi hili la joto la siku tano