Wafanyabiashara nchini Uganda wameridhia kufungua tena bishara zao, baada ya rais Yoweri Museveni kuagiza mamlaka ya kutoza kodi kusimamisha kwa muda mamlaka hiyo kuacha kuwaadhibu wafanyabiashara waliolemewa kulipa kodi kutumia mfumo wa kigitali unaojulikana kama EFRIS, Kitengo cha habari cha rais kimebaini.

Uamuzi huu ulifikiwa katika mkutano baina ya viongozi wa mashirikisho ya biashara na rais Museveni kufuatia mgomo wa siku nne wafanyabishara kufunga maduka na shughuli za biashara katika mji mkuu Kampala na baadhi ya miji nchini humo wakipinga kodi nyingi kwa biashra wanazoaigiza kutoka nje mwa nchi hiyo.

Katika mkutano huo, wamesema watafungua biashra hizo huku viongozi wao wakiendelea kufanya mazungumzo na serikali kabla ya kukutana tena na rais ifikapo Mei 7.