DAR ES SALAAM: RAIS Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi katika nafasi mbili tofauti ambapo amemteua Ramadhani Lwamo kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini. Kabla ya uteuzi huo, Mhandisi Lwamo alikuwa akikaimu nafasi hiyo.
Taarifa iliyotolewa leo Januari 15, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu, Balozi Dk Moses Kasiluka kupitia Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Sharifa Nyanga imeeleza kuwa Rais amemteua pia Dk Aggrey Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Ushindani (FCC) kwa kipindi cha pili.Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa Rais Samia Profesa Othaman Chande Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kipindi cha pili.
Rais Samia pia amemteua Dk Florens Taruka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania ( TFC) kwa kipindi cha pili.
Aidha Prof Velerian Silayo ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kituo cha Zana za Kilimo na Teknolojia Vijijini ( CAMERTEC) kwa kipindi cha pili.
0 Comments