Lionel Messi ameshinda mataji 44 kwa klabu na nchi

Akiwa ametoka kuiongoza Inter Miami katika ushindi wa kihistoria wa Kombe la MLS, Messi anaelekea India kwa ziara ya siku tatu.

Akiongozana na wenzake wa klabu hiyo Luis Suarez na Rodrigo de Paul, mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d'Or atazindua sanamu yake huko Kolkata Jumamosi.

Imetengenezwa kwa muda wa siku 27 na wafanyakazi 45 na ina urefu wa futi 70.

Ziara inaanza Kolkata asubuhi siku ya Jumamosi, kabla ya kuelekea Hyderabad, Mumbai na Delhi.

Sanamu hiyo ni sehemu ya heshima ya India kwa fowadi huyo wa zamani wa Barcelona na Paris St-Germain.

Messi, ambaye amefunga mabao 787 katika mechi 963 katika ngazi ya klabu, alitunukiwa sanamu ya shaba huko Buenos Aires, Argentina, mwaka 2016.

Rais wa Barcelona Joan Laporta hivi majuzi alisema "wanafanyia kazi" sanamu ya Messi huko Nou Camp.

o

CHANZO CHA PICHA,EPA

Maelezo ya picha,Makumbusho binafsi ya Cristiano Ronaldo yana kumbukumbu na tuzo kutokana na kazi yake

Mwaka 2014, mpinzani wake wa muda mrefu Ronaldo alizindua sanamu yake katika jumba la kumbukumbu yake huko Funchal kisiwa cha Madeira, Portugal.