Mwanaume anaangalia ratiba ya treni kwenye skrini katika stesheni ya reli ya Entrecampos siku ambayo vyama vikuu viwili vya wafanyakazi, CGTP na UGT, viliitisha mgomo dhidi ya mpango wa serikali wa kurekebisha sheria za kazi, huko Lisbon, Ureno, Desemba 11, 2025.

Huduma za treni zimesimama kote Ureno siku ya Alhamisi, mamia ya safari za ndege zimekatishwa, na shule zimefungwa baada ya vyama vya wafanyakazi kuanzisha mgomo mkubwa katika zaidi ya muongo mmoja, kupinga mapendekezo ya mageuzi ya kazi.

Serikali ya wachache ya mrengo wa kati wa kulia inasema mabadiliko yaliyopendekezwa – ya kurekebisha zaidi ya vifungu 100 vya kanuni za kazi - yanalenga kuongeza tija na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Lakini vyama vya wafanyakazi vinasema mabadiliko hayo yanawapa madaraka waajiri kwa gharama za kukandamiza haki za wafanyakazi, licha ya uchumi imara na wingi wa ajira.

Mswada huo ambao bado haujawasilishwa bungeni, unatarajiwa kupitishwa kwa kuungwa mkono na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Chega.

"Tutakuwa na mgomo mkubwa, wito wetu ni kwa kila mfanyakazi kutumia siku hii kama njia ya kukataa mageuzi ya kazi," Tiago Oliveira, katibu mkuu wa muungano wa vyama vya CGTP, aliwaambia waandishi wa habari.

Huu ni mgomo mkubwa tangu Juni 2013, wakati Ureno ilipochukua hatua kali za kubana matumizi