Jopo muhimu la bunge la Marekani limepiga kura ya kumshutumu Rais wa zamani Bill Clinton na mkewe, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton, kwa kudharau Bunge kutokana na kukataa kwao kuitika wito katika uchunguzi wake dhidi ya Jeffrey Epstein wa aliyehukumiwa kwa uhalifu wa makosa ya ngono.
Kamati ya Usimamizi ya Baraza la Wawakilishi inayoongozwa na Republican iliidhinisha hatua hiyo ya dharau, kwa kuungwa mkono na Wademokrasia kadhaa, na sasa itapelekwa kwa Baraza lote la Wawakilishi kwa ajili ya kupigiwa kura.
Ikiwa itapitishwa na baraza la wawakilishi, suala hilo litapelekwa kwenye wizara ya sheria. Kamati hiyo ilikuwa imewaita wote wawili kutoa ushahidi kuhusu Epstein, ambaye Bill Clinton ameonekana naye kwenye picha katika miaka ya 1990 na mwanzoni mwa miaka ya 2000.

0 Comments