Waziri wa masuala ya Polisi wa Afrika Kusini Firoz Cachalia amesema kwamba vikosi vya usalama bado havijaweza kupambana na magenge hatari ya wahalifu, katika kukiri waziwazi kunakoonesha ukubwa wa tatizo la uhalifu nchini humo.
Ghasia za magenge, pamoja na wizi, zinachangia mauaji mengi nchini Afrika Kusini, ambayo ina moja ya viwango vya juu zaidi vya mauaji duniani.
Cachalia alisema vurugu za magenge zimezidi kuwa ngumu, hasa katika majimbo ya Eastern Cape na Western Cape, zikihitaji mikakati mipya zaidi ya polisi wa jadi. "Siamini kwamba kwa sasa tuko katika nafasi ya kushinda magenge haya," waziri huyo aliwaambia waandishi wa habari Jumatano.
Afrika Kusini, taifa lenye viwanda vingi zaidi barani Afrika, imekuwa ikipambana na uhalifu uliojikita zaidi.
Watu wengi nchini Afrika Kusini wanamiliki bunduki zenye leseni kwa ajili ya kujilinda, lakini kuna bunduki nyingi zaidi haramu zinazosambazwa.
Data ya polisi inaonesha kwamba wastani wa watu 63 waliuawa kila siku kati ya Aprili na Septemba mwaka jana.

0 Comments