Rais Donald Trump akizungumza kuhusu mashambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran mwaka jana, ambayo alisema "iliharibu kabisa" uwezo wa nyuklia wa nchi hiyo.

"Iran inataka kuzungumza, na watazungumza," Trump aliongeza, kabla ya kuendelea kuzungumzia operesheni dhidi ya kundi linalojiita Islamic State (ISIS) nchini Syria.

Trump kisha akasema kwamba "mambo mengi mazuri yanatokea," na akaelezea jinsi vitisho kwa Ulaya, Marekani na Mashariki ya Kati "vinapungua au kupungua." "Mwaka mmoja tu uliopita ulimwengu ulikuwa unawaka kihalisi, na watu wengi hawakujua," aliongeza.

Kulingana na afisa wa zamani wa Pentagon, kutokana na kupungua kwa maandamano ya barabarani, Marekani inaweza kuendeleza sera ya shinikizo kwa kutishia rasilimali za mafuta za Iran ili kuirudisha Iran kwenye meza ya mazungumzo, badala ya kuchukua hatua moja kwa moja.

"Ikiwa watu hawapo mitaani, itakuwa vigumu sana kufanya shambulizi na hiyo ndio changamoto," anasema Mara Carlin.

"Kundi la meli za kubeba ndege huenda likawasili katika eneo hilo katikati ya wiki ijayo, na labda ikiwa mambo yanaonekana kuwa shwari na watu hawapo mitaani, meli zitakaa katika eneo hilo kama kizuizi."

Kinachoonekana kuwa na uhakika hadi sasa ni kwamba Donald Trump si wa kawaida katika maamuzi yake. Wakati wa vita vya siku 12, awali alisema Marekani haitashiriki katika shambulio dhidi ya Iran, lakini ghafla akaamuru shambulio dhidi ya vituo vya nyuklia vya Iran.

Mwaka uliopita, kulingana na shirika la "Armed Conflict Events and Locations Database" (ACLED), Marekani imefanya mashambulizi 626 ya anga katika nchi mbalimbali duniani kote, ikiwa ni pamoja na Somalia, Iran, Yemen, Nigeria, Venezuela, Iraq na Syria, yote yalifanywa kwa idhini ya rais wa Marekani.

Mara Carlin anasema, kwa marais waliopita unajua wakati serikali iko tayari kutumia nguvu za kijeshi na wakati ambapo haitaki kutumia nguvu za kijeshi. Lakini kwa Rais Trump, kila kitu hakina uhakika na ni vigumu sana kutabiri."