
MASHINDANO ya Tuzo za Kimataifa za Qur’an Tukufu yanatarajiwa kufikia kilele Aprili 5, huku washiriki kutoka mataifa 25 wakianza kuwasili nchini kushiriki tukio hilo la kidini. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Othman Kaporo amesema maandalizi yamekamilika na mapokezi ya washiriki yameanza, huku ujio wao ukitarajiwa kuendelea hadi Ijumaa.
Amesema hatua ya nusu fainali itafanyika katika ukumbi wa Golden Tulip Hotel kuanzia asubuhi hadi jioni, ambapo washiriki bora watachujwa kuingia fainali. Kaporo amesema fainali zitafanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kuwakaribisha Watanzania kujitokeza kwa wingi kushuhudia tukio hilo.
Ameongeza kuwa mashindano hayo yatapambwa na uwepo wa viongozi wa kidini kutoka nje ya nchi, wakiwemo Maimamu kutoka Makkah na Madina, huku yakisimamiwa na majaji wa kimataifa. SOMA: Watakaowahi mashindano ya Quran kupewa zawadi
Kwa upande wake, Sheikh Hassan Chizenga, kwa niaba ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakari bin Zubeir amewataka Watanzania kujitokeza kushiriki mashindano hayo, akisema yanaimarisha mshikamano na maadili ya jamii.
0 Comments