ZANZIBAR; RAIS wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan, ameipongeza klabu ya Simba kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano baada ya kuifunga Yanga bao 1-0 katika mchezo wa fainali jana Uwanja wa New Amaan Complex mjini Unguja.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa mtandao wa Instagram, Rais Samia ameandika: “Ninaipongeza Klabu ya Simba kwa kutwaa ubingwa wa Kombe la Muungano mwaka 2026. Mbali na burudani, michezo imeendelea kuwa daraja imara linalotuunganisha.

“Pia, ninazipongeza klabu zote nane zilizoshiriki mashindano hayo kwa kuonesha ushindani wa kirafiki na hamasa inayozidi kuimarisha tunu ya Muungano wetu.”