Andy Burnham

Andy Burnham amepiga hatua ya kukaribia kuwa kiongozi mpya wa Chama cha Labour na Waziri Mkuu wa Uingereza, baada ya kupata uungwaji mkono wa idadi kubwa ya wabunge wa chama hicho ili kumrithi Keir Starmer.

Ombi la Burnham la kuwania uongozi wa Labour limeungwa mkono na wabunge 322 kati ya 403 wa Labour, huku akiwa mgombea pekee aliyetangaza nia ya kugombea nafasi hiyo.

Hii ina maana kwamba anahitaji uteuzi mmoja tu zaidi kufikisha idadi ya wabunge 323, ambayo itawafungia nje wagombea wengine kuingia katika kinyang'anyiro hicho.

Baadhi ya wabunge wamesema hawakuweza kupiga kura Alhamisi, lakini watamuunga mkono Burnham watakaporejea bungeni.

Iwapo hakuna mgombea mwingine atakayejitokeza, Burnham atatangazwa rasmi kuwa kiongozi wa Labour wiki ijayo kabla ya kuapishwa kuwa Waziri Mkuu tarehe 20 mwezi Julai.

Awali Burnham, amewahi kuwa meya wa Greater Manchester, kabla ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa eneo la Makerfield.